Watoto na Yesu App
App hii itamfundisha mtoto wa Kikristo Neno la Mungu kwa furaha kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili asiliache Neno la Mungu hata atakapokuwa mkubwa katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia, zipo namna nyingi za kujifunza nasi tumepata neema kufikisha mafundisho ya wototo kwa njia hii. App hii pia itampa mwalimu wa Shule ya Jumapili mwongozo wa somo, Neno la Biblia, mifano katika picha, video, michezo na nyimbo kwa urahisi na kufurahisha.